Habari

Video: GeoPoll yatemwa na Ofisi ya Takwimu (NBS)

Ofis ya Takwimu imesema kuwa hivi karibuni kumekuwa na takwimu zinazotolewa na Kampuni ya GeoPoll yenye Ofisi ya Kanda ya Afrika Mjini, Nairobi Kenya. Takwimu hizo ambazo hutolewa kwa njia ya mitandao ya kijamii, zinahusu ukusanyaji wa taarifa za Televisheni na Redio nchini kwa idadi ya watazamaji na zinatolewa kila baada ya miezi mitatu.

Akizungumza na waandishi wa Habari, Mkurugenzi Mkuu, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS),Dk Albina Chuwa amesema kuwa takwimu hizo sio Takwimu Rasmi (Official Statistics) kwa kuwa hukusanywa kwa mfumo ambao hautambuliwi na NBS kwa mujibu wa kifungu cha 20 cha Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015.

Hata hivyo NBS inaitaka Kampuni ya GeoPoll kufuata taratibu zilizoainishwa katika Sheria ya Takwimu, kwa kuwa takwimu zinazotolewa na kampuni hiyo hazijakidhi vigezo vya Takwimu Rasmi na zinapotosha umma na kuleta mkanganyiko kwa wadau pamoja na kuathiri mahusiano ya kiutendaji baina ya vyombo vya habari hapa nchini.

Aidha NBS imeongeza kuwa kwa mantiki hiyo, takwimu zinazotolewa na mtu au taasisi yoyote bila kufuata au kukidhi vigezo vinavyotolewa na NBS kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu, hazitambuliwi kuwa ni Takwimu Rasmi na kwa maana hiyo haziwezi kutumika katika kupanga mipango ya maendeleo ya nchi.

Video:

Na Salum Kaorata & Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents