Habari

Video: Lady Gaga na R.Kelly ni kati ya wasanii waliofanya show ya kuvutia zaidi katika AMA 2013

Lady Gaga ni miongoni mwa watu waliovutia macho ya watu wengi waliohudhuria na waliofuatilia online tuzo za ‘American Music Awards 2013’ jana, kuanzia style aliyoitumia kuingilia red carpet (mfano wa farasi), na baadaye kufanya show ya kiubunifu ya collabo yake na R.Kelly ‘Do What You Want’.

Kelly n Gaga

Performance yao ilianza kwa mtindo wa igizo, pale Gaga alipogeuka ‘Sexy secretary’ na R.Kelly akageuka kuwa Rais, tukio ambalo kwa mujibu wa Daily Mail lilirudisha hisia za uhusiano wa miaka ya 90 kati ya Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton na Monica Lewinsky.

Gaga akiwa katika meza yake kama secretary anapokuwa ofisini huku R.Kelly akiwa katika meza yake ya Rais ikiwa na bendera ya Marekani vyote vikifanyika jukwaani.

Gaga anaonekana yuko busy akipokea simu zinazoingia mfululizo na kujibu “American Music Awards hold please”, mpaka simu ya nne anayoipokea na kugundua kuwa ni Rais ‘Kelly’ kwa mshituko anasimama na kujibu “Oh president Kelly”, huku Kelly ambaye ndiye ameipiga simu hiyo anamjibu kwa kuimba “ Hurry up I had a bad day, can you bring me my lunch”, Gaga anamjibu kwa kuimba pia, “What are you hungry for mr President”, R.Kelly anamjibu “girl you have been working for me for six long years, you know what I want”.

Tazama performance hiyo iliyoongeza utamu wa tuzo hizo jana

http://youtu.be/qva7OuYe8pk

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents