Habari

Video: ”Matarajio yangu Membe atarudi CCM, nikiwa hai au nimekufa,”- Dkt. Bashiru Ally

Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally amesema anaimani kwamba Membe atarudi CCM, kwa sababu milango ya wanachama waliofukuzwa CCM ipo wazi kuomba radhi na kusamehewa, kwani kwa uzoefu wake tangu afike CCM ameshasaini barua za misamaha 14, hivyo anasubiri ya 15 ya Bernad Membe kama akitaka.

Dkt. Bashiru Ally amesema kuwa ”Mzee Makamba alihojiwa na ushahidi upo, wote walipata nafasi kwa mujibu wa kanuni, kujieleza, kujitetea, walifika mbele ya kamati na ushahidi upo.”

”Mimi namtakia maisha marefu, na matarajio yangu ni kwamba atarudi CCM nikiwa hai au nikiwa nimekufa, kwa sababu milango ya kuwapokea wanachama wapya ipo wazi. Na milango ya wanachama kuondoka kwa hiyari iko wazi, na milango ya wanachama waliyo fukuzwa kuomba radhi wakasamehewa iko wazi,” amesema Dkt. Bashiru

”Katibu huyo Mkuu wa CCM ameongeza ”Mimi tangu nimefika nimesha saini barua za misamaha ya walio fukuzwa 14 nasubiri ya 15 ya Membe kama akitaka nitaisaini tu.”

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents