Habari

Wasimamizi wa sekta ya fedha wazindua daftari la kudumu la watoa huduma za kifedha (FSR)

Wasimamizi wa sekta ya fedha Tanzania wakiungwa mkono na Mfuko wa kuendeleza sekta ya Fedha Tanzania, wamezindua Daftari la kudumu la watoa huduma za kifedha , ambalo lengo ni kuonyesha mahali ambapo vituo vinavyotoa huduma za kifedha vinapatikana kwenye nchi.

FSR ni daftari endelevu ambalo litaonyesha mahali ambapo vituo vinavyotoa huduma za kifedha vinapatikana kwa nchi nzima kwa kukamata tarakimu za kijiografia zinazoonyesha eneo na aina ya huduma inayopatikana ambalo lengo lake ni kufungulia uwezo wa takwimu za kijiografia kama kifaa kwa ajili ya intelijensia ya kibiashara, kufanya maamuzi na mipango mikakati.

Wasimamizi wakiongozwa na Benki kuu ya Tanzania inajumuisha Tume ya maendelo ya ushirika (TCDC), Mamlaka ya usimamizi wa bima Tanzania (TIRA) na Mamlaka ya masoko ya mitaji na dhamana (CMSA).

Benki kuu ya Tanzania pamoja na mwenyekiti wa Tume ya taifa ya huduma jumuishi za kifedha, Profesa Florens Luoga, alizindua mfumo wa daftari la kudumu la watoa huduma za kifedha kwa kukuza kauli mbiu ya “Takwimu ni Mafuta mapya” na ambao wataitumia ipasavyo na kwa manufaa yao watavuna matunda yake na kukua”

Alisema kuwa daftari la kudumu la watoa huduma za kifedha italeta machine ambayo itakusanya na kufungulia nguvu ya takwimu ili kuhimiza ukuaji, ubunifu na ushirikiano ndani ya sekta ya fedha Tanzania ambayo iko tayari kwa ajili ya muongo huu wa kidijitali, viwanda na muunganisho

Mwishowe, aliitisha ushirikiano baina ya wadau wote wa sekta na mawakala binafsi na wamiliki vituo vya huduma kuhakikisha uandikishaji/usajili utaoenda vizuri na kufanikiwa na hivyo kwa ajili ya kuboresha sekta ya fedha

FSR itakuwa daftari la kwanza la aina yake katika nchi za afrika chini ya jangwa la sahara ambalo litaendesha lenyewe mchakato wa kukusanya takwimu na kutoa upatikanaji wa taarifa kwa kidijitali moja kwa moja. Ingawa daftari litatumika kama mfumo wa taifa wa kufuatilia ukuaji na mgawanyo wa vituo vinavyotoa huduma za kifedha na kuwataarifu wadau wakuu wa Mpango wa taifa wa huduma jumuishi za kifedha kwa mwaka 2018-2022 na umma kwa ujumla.

Kwa kuongezea, FSR itatoa taarifa za kimkakati kwa watoa huduma za kifedha ili kuhakikisha mahitaji ya mlaji yanakidhiwa na huduma zinaletwa karibu na makundi halisi ya walaji.

Benki kuu ya Tanzania imechukua uongozi wa utekelezaji wa FSR kwa sababu ya jukumu lao kubwa kwenye sekretarieti ya mpanngo wa taifa wa huduma jumuishi za kifedha na jukumu lao kama msimamizi wa sheria ya fedha kwa kielekroniki. Mfumo uliundwa na wasanidi kutoka benki kuu ya Tanzania.

Kati ya Februari na Juni 2020, Benki kuu ya Tanzania itatuma timu ya wakusanya taarifa nchi nzima ili kusajili vituo vinavyotoa huduma za kifedha. Hii itajumuisha matawi ya benki, machine za kutolea na kuweka fedha, wakala wa benki na wafanyabiashara, wakala wa huduma ya pesa kwa simu za mkononi na wafanyabiashara, SACCOs, Benki ndogo za biashara na taasisi pamoja na madalali wa bima, mawakala na madalali wa masoko ya dhamana na washauri walioteuliwa usajili huu utafanyika kupitia program ya simu inayoitwa FSR collect ambayo inapatikana kwenye simu zenye mfumo wa android ambayo imetengenezwa na Benki kuu ya Tanzania. Kila kituo kitakachosajiliwa kitapewa kitambulisho cha FSR, cheti ambacho kina namba zinazoweza kusomwa na binadamu na kodi ya QR, ambacho kitatakiwa kuweka sehemu inaonekana kwenye kituo

Takwimu zitapatikana katika ngazi mbalimbali za watumiaji, umma, watoa huduma za kifedha na wasimamizi. Mwanzoni maeneo ambayo huduma zinapatikana yataonyeshwa lakini miezi ijayo hapo mbeleni takwimu mpya vipengele vitaongezewa. Hii itajumuisha uwezo zaidi wa kuchanganua takwimu ikihusisha takwimu nyingine za kijamii na kiuchumi kama vile huduma za kijamii, elimu na huduma ya afya pamoja na uhusiano na shughuli za kiuchumi katika eneo hiyo ni masoko ya kilimo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents