Burudani

Video: Octopizzo aperform show ya Kenya kwa Skype akiwa Ulaya

Umbali sio kikwazo tena mbele ya teknolojia, ndio maana rapper wa Kenya Octopizzo ameweza kusuuza nyoyo za mashabiki wake wa nyumbani (Kenya) kwa kutumbuiza kwa njia ya Skype huku yeye akiwa ziarani Ulaya.

pizzo2

Kilichotokea ni kuwa kundi la Elani lilifanya show Kenya weekend iliyopita, na miongoni mwa nyimbo walizoimba ni pamoja na collabo yao mpya waliyofanya na Octopizzo. So kilichofanyika ni kwamba Octopizzo ambaye yuko Ulaya aliunganishwa kwenye screen kubwa iliyopo ukumbini hapo na ku-perform verse yake, na kupata shangwe za kutosha kutoka kwa mashabiki waliohudhuria show.

Octopizzo alishare kipande cha video ya show hiyo na kuandika;

“S/O to #Elani on their dope performance today,I had to Perform our #BrandNew Collabo Via #Skype all the way from Europe coz I have no days off,I be doing shows in the 254 even when am out of town”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents