Burudani

Video: Pharrell Williams alivyowasha moto kwenye 2014 NBA All Stars, Diddy, Busta, Nelly, Snoop wampa kampani

Kabla ya mechi ya wachezaji bora wa NBA kuingia kwenye mechi ya Jumapili ya All-Star Game, Pharrell Williams alitumbuiza kwa dakika 20 na kupewa kampani na mastaa wenzie. Producer na muimbaji huyo alianza kwa wimbo wake wa mwaka 2003, “Frontin’ kabla ya Nelly kuungana naye na kuimba pamoja wimbo ‘Hot in Here’ na kisha kufuatiwa na “I Just Wanna Love U (Give It 2 Me).”

http://www.youtube.com/watch?v=edEg_aJch28#t=235

Diddy na Busta Rhymes walimsaidia kuimba Smoothie King Center na “Pass the Courvoisier, Part II. Lakini wakachanganya na mashairi ya ‘Pass the Ciroc this way’. Snoop Dogg alipanda kuimba naye “Beautiful,” na wachezaji wa Western Conference wakaingia uwanjani wakati wakitumbuiza “Drop It Like It’s Hot.”

Mwisho, Pharrell akamalizia na “Get Lucky” kabla ya kufunga na “Happy” wakati Diddy, Busta, Nelly na Snoop wakicheza kwenye jukwaani.

“No words for how grateful I am these legends joined me 2nite,” alitweet Pharrell.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents