BurudaniVideos

Video: Raymond akiri kuzama ‘penzini’ kwa Avril wa Kenya, amuambia mbele ya mashabiki Mombasa

Raymond ameamua kuusemea moyo wake mbele ya mashabiki maelfu kwenye show ya WCB, Mombasa, Kenya.

14134680_1356178264394096_1789614729_n

Muimbaji huyo wa ‘Kwetu’ alimpandisha jukwaani mrembo wa Kenya, Avril na kumuimbia wimbo maalum kuelezea hisia zake waziwazi kuwa ni msichana anayempenda na kuwaacha mashabiki wakiangusha shangwe za kutosha.

Hakuuishia hapo, Ray alipost picha akiwa na Avril na kuandika: Trust me @theavieway I really love you … thanks for coming … God bless you.”

Avril naye alionesha kudata kwelikweli na dogo huyo kwakuwa hakuisha kupost picha na video za show yake.

“This song that @rayvanny serenaded me with should be my next collabo hmmmm #ThinkingOutLoud,” aliandika kwenye picha aliyoweka Instagram akiwa na mkali huyo wa freestyle.

14072810_1764651553773059_600693094_n

Hadi sasa tunafahamu kuwa Avril yupo single baada ya kuachana na mpenzi wake Msouth na pia Ray hajawahi kuonesha kuwa na msichana yeyote na hivyo wawili hawa wanaweza kuwa ‘perfect combo.’

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Raymond, Harmonize na Rich Mavoko walikuwa na show kwenye mjini wa mwambao wa Mombasa nchini Kenya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents