Burudani

Video: Studio mpya ya Hanscana ‘Wanene Films’ kukamilika mwezi April, imegharimu zaidi ya Bilioni 1

Muongozaji wa video na mshindi wa Tuzo za Watu, Hanscana amesema studio yake mpya ‘Wanene Films’ iliyopo Mikocheni B jijini Dar es salaam itaanza kufanya kazi rasmi mwezi April mwaka huu.
Hanscana akiwa katika studio yake

Akizungumza na Bongo5 Jumatatu hii akiwa katika ofisi hiyo mpya, Hanscana alisema studio hiyo imechukua miaka 3 mpaka kukamilika huku akidai imegharimu bilioni 1.

“Ingawa ipo kwenye hatua za mwisho lakini bado hatuja kaa chini kuangalia gharama ni kiasi gini, ni hela nyingi kusema kweli kwa sababu hata contractor aliyedesigner hii studio ni mfaransa na mpaka leo duniani ameshadesigner studio 104, 3 Afrika, moja hii hapa, nyingine zipo Misri. Pia huyu jamaa ni mhadhiri mkuu wa chuo kikuu cha Cambridge. Pia kuna contractor anayejenga hii project ametokea Afrika Kusini, kuna contractor wa Ufaransa, kuna contractor wa India, Kwahiyo sasa hivi tunaongelea 1 Billion,” alisema Hanscana.

“Kwa sababu hili godauni unadhani ni shingapi?. Toka tumelichua huu ni mwaka wa watatu na bado tunaendelea na ujenzi. Kila mwezi tunalipia umeme, kodi ingawa pia tuna jenereta letu kubwa. Pia tunawalipia macontractor kula na kulala na wanalala hotel ya 5 Star.,” aliongeza Hanscana.

Pia Hanscana alizungumzia uhusiano yake na kampuni ya Wanene Film ambayo anashirikiana nayo katika maandalizi ya studio hiyo.

“Unapo zungumzia Wanene na Hanscana, kuna position mbili, kuna ‘Wanene Film’ ambayo ndio mimi, ipo under Hanscana mwenyewe. Alafu kuna ‘Wanene Studio’ ambayo ina mambo ya recording, chini ya meneja Dashi ambaye ni CEO wa hii kitu. Kati yangu mimi na Wanene tumeinvest the same, hela imeingia, mimi pia nimeinvest talent yangu ndio maana kila video unaona kuna Wanene.,” alisema Hanscana

Angalia hapa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents