Burudani

Video: Taylor Swift na Future walivyotengeneza kichupa cha ‘End Game’

Je unatamani kuiona video ya wimbo mpya ‘End Game’ wa Taylor Swift ambao amemshirikisha Future na Ed Sheeran? Basi unatakiwa kukaa mkao wa kula.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, umeonyesha kipande cha video ya wasanii hao wakionekana kuwa location kwa ajili ya kutengeneza video hiyo.

Inadaiwa kuwa video hiyo imeanza kutengenezwa Jumanne hii huko mjini Miami katika boti kubwa lakini msanii Ed Sheeran hakuwepo katika eneo hilo.

https://youtu.be/9X7i71W4sQk

Wakati huo huo inadaiwa kuwa kuna uwezekano msanii Katy Perry akaonekana katika video hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents