Michezo

Video: Tazama mpishi maarufu wa nyama ‘Salt Bae’ alivyowakutanisha Pogba na Messi Dubai

Mpishi maarufu wa nyama wengi wakimtambua kama mfalme wa kuoka nyama anayefahamika kwajina la Nusret Gökçe maarufu ‘Salt Bae’ Ijumaa hii alikuwa mwenyeji wa nyota wawili wa soka Lionel Messi na Paul Pogba wakiwa pamoja na kuwatengenezea chakula hicho huko Dubai.

 

Salt Bae ambaye ni raia wa Uturuki ameposti vipande vya video kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram vikionyesha akiwa na nyota hoa maarufu katika ulimwengu wasoka huku akiwatengenezea msosi wa nyama.

Kufuatia kupata chakula hicho cha jioni, Messi na Pogba walipata nafasi ya mazungumzo ya muda mrefu huku wakifurahia nyama walizoandaliwa na Mturuki huyo ‘The Meat King’.

Inasemekana sehemu ya mazungumzo hayo ni pamoja na kiungo huyo wa Man United, Pogba kuamia Barcelona.

Ni kawaida kwa mgahawa wa Nusr-Et kushuhudia wageni mbalimbali maarufu wakiwemo wanamuziki, wachezaji na hata wasanii filamu kutoka pande zote za dunia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents