Burudani

Video: Wema nusura avunje interview baada ya kuona Idris anatoweka kwenye himaya yake

Tamasha kubwa la muziki la fiesta lililofanyika weekend iliyopita katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es salaam lilikuwa na matukio mbalimbali. Lakini tukio ambalo limesambaa katika mitandao ya kijamii ni lile ambalo linamuonyesha malkia wa filamu, Wema Sepetu akiwa karibu aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Idris Sultan.
wema

Katika video hiyo ya sekunde 47 iliyosambaa mtandaoni, inamuonyesha Wema akihojiwa na Clouds TV lakini mahojiano hayo yalitaka kuvunjika muda mfupi baada ya malkia huyo wa filamu kuona Idris Sultan akitoweka katika eneo ambalo alikuwa mwanadada huyo.

Mashabiki wa mwigizaji huyo katika mitandao ya kijamii wamekuwa na maoni tofauti tofauti huku wengi wakidai huwenda wawili wao bado wanaendelea kimya kimya.

Wawili hao ambao mapenzi yao yalikuwa moto moto miezi kadhaa iliyopita kabla ya kudaiwa kuachana, hakuna aliyeweza kuweka wazi juu ya sababu ya kuachana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents