Burudani

Video ya ‘Don’t Bother’ imegharimu milioni 32 – asema Joh Makini

Mara nyingi wasanii wengi wa Bongo huwa hawapendi kutaja gharama walizotumia kwenye kazi zao hususan video wanazofanya, na kila mmoja huwa anasababu zake tofauti za kutotaka kusema ametumia kiasi gani.

Johmakini.1

Rapper wa Weusi, Joh Makini ambaye hivi sasa wimbo wake mpya ‘Don’t Bother’ umekuwa ‘talk of the town’ toka alipoachia video Alhamisi, iliyofatiwa na audio iliyotoka siku ya Ijumaa (Nov 13) ametaja gharama iliyotumika kukamilisha video hiyo.

Joh makini amesema video hiyo iliyofanyika Afrika Kusini na kuongozwa na Justin Campos wa Gorilla Films imegharimu jumla dola 15,000 sawa na takribani shilingi milioni 32 za Kitanzania.

“Kwa level ambazo naenda za kimataifa natakiwa kulipa pesa kubwa kwa video, gharama ya don’t bother ni dola 9000, including models na production, lakini ukiongeza na shopping zetu mavazi na vingine jumla dola 15000” alisema Joh kupitia Planet Bongo ya East Africa Radio.

Joh ameongeza kuwa video hiyo imevunja rekodi ya video zake zote alizofanya.

“Nimevunja tena rekodi yangu, ngoma ya ‘Don’t Bother’ imeshacross ni moja ya ngoma inayotrend kwenye tasnia ya muziki ya South Africa”, alisema Joh Makini.

Hadi leo Nov 14 video ya ‘Don’t Bother imetazamwa mara 59,185 toka ilivyowekwa Youtube Nov 11, 2015.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents