Michezo

Video: Zaidi ya watu elfu 45 waudhuria mchezo wa Everton – Sportpesa

Wiki iliyopita Tanzania ilishuhudia ziara kubwa ya klabu ya Everton inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza kuwasili nchini na kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Gor Mahia ya Kenya.

Mkurugenzi wa Kampuni ya michezo ya kubashiri matokeo ya Sportpesa , Abbas Tarimba

Mkurugenzi wa Kampuni ya michezo ya kubashiri matokeo ya Sportpesa , Abbas Tarimba amewashukuru wa Tanzania kwa kuonyesha uzalendo na ushirikiano wa hali ya juu katika kipindi chote ambacho Everton walikuwepo nchini.

Akizungumza na vyombo vya habari leo, Tarimba amesema zaidi ya watu elfu thelathini na tisa (39) walilipa viingilio kwaajili ya kwenda kushuhudia mchezo huo huku ukiongeza idadi ya watu waliyopata tiketi kupitia promosheni unapata jumla ya watu elfu arobaini na tano (45) hivyo inaonyesha kwa kiasi gani watu walijitokeza kwa wingi licha ya wale ambao waliendelea kuingia hata katika dakika za mwisho.

Tarimba ameongeza kwa kuishukuru Ofisi ya rais Ikulu na ya Makamu wake kwa kutoa ushirikiano mkubwa na hii inaonyesha serikali ya awamu ya tano ipo pamoja na michezo.

Wakati huo huo bosi huyo wa Sportpesa amelishukuru Jeshi la polisi kwa ushirikiano mkubwa waliyouonyesha pamoja na Wizara ya Mambo ya Nje na Wizara ya Mambo ya Ndani kwa kuonyesha ushirikiano mkubwa.

By Hamza fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents