Burudani

Vita ya dawa za kulevya: 12 kati ya 112 kupandishwa kortini akiwemo Wema, TID na wengine (Video)

Sakata la Madawa ya kulevya limeendelea kugonga vichwa vya habari wiki hii ambapo Jumatatu hii Jeshi la polisi limedai toka lianze operesheni hiyo tayari limewakamata watuhumiwa 112 na kati ya hao 12 watapandishwa mahakamani Jumatatu hii kwajili ya kiapo cha kutorudia matumizi ya Madawa ya kulevya baada ya kukiri kutumia.

Kati ya watu hao 12 ni pamoja na Wema Sepetu, Romy Jones, Petit Man, TID pamoja na wengine.

Aidha Wema Sepetu baada ya kiapo hicho atarudishwa polisi kwajili ya kuandaliwa shtaka jipya linalomkabili la kukutwa na msokoto wa bangi nyumbani kwake.

Akiongea na waandishi wa habari Jumatatu hii, Kamanda wa Polisi wa Kanda maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema watuhumiwa wengi waliohojiwa walikiri kutumia Madawa ya kulevya na kati ya hao walieleza watu ambao wanawauzia.

“Tumewakamata watuhumiwa jumla 112 na tumekamata kete 299 zinazodhaniwa ni za Madawa ya kulevya na kwa kawaida haya Madawa Mkemia Mkuu wa serikali yeye ndiye atakayetuambia ni Madawa ya aina gani,” alisema Kamanda.

Aliongeza, “Katika watuhumiwa 112, kuna watuhumiwa 12 tunawapeleka leo mahakamani, tunawapeleka mahakamani kwa sababu sheria ya mwenendo wa mashtaka iko wazi kifungu cha 73 na 74, huwa tunaweza kuomba kwa mweshimiwa hakimu kuwaombea watuhumiwa kwa kiapo, kwamba hawa watuhumiwa tunataka wabadilishe tabia zao. Tunawapeleka mahakamani ili wache chini ya uangalizi wa jeshi la polisi na mahakama kwa muda wa miaka 2 wasifanye makosa tena,”

“Kwa sababu tulichokibaini kwa wote tuliowakamata wengine wanakiri na wamekwenda kuonyesha hayo Madawa ya kulevya. Kwa hiyo kusudio la kwanza wawe chini ya uangalizi wetu, na kusudio la pili la kiapo chetu waache hiyo tabia ili wabadilike wawe raia wema, lakini la tatu tumeomba wale wanakuja kuripoti kituoni angalau mara mbili kwa mwezi na lengo letu ni kuona hawa ndugu zetu ambao walikiwa wanavuta madawa ya kulevya wamecha kabisa,”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents