Habari

Vita ya dawa za kulevya: RC Makonda aungwa mkono na Ubalozi wa Ujerumani (Video)

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ametembelewa ofisini kwake na balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Deltet Waechter  na kujadili mambo mbalimbali ya mkoa wa Dar es salaam.

RC Makonda amesema kuwa wamekubaliana kushirikiana katika mapambano ya Biashara ya Dawa za kulevya pamoja na kutoa mafunzo ya namna ya kulinda Jiji kwa kutumia Teknolojia.

Aidha RC Makonda amewasilisha kwa Balozi huyo ombi la kujengwa kwa Jengo la huduma ya Dharura (ICU) kwenye Hospital za Mkoa wa Dar es salaam ambapo Balozi amelichukuwa ombi hilo kwaajili ya kulifanyia kazi.

Balozi wa Ujerumani Nchini Bwana Deltet Waechter amesema watashirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa katika masuala yote ya Maendeleo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents