Burudani

Vitu gani wasanii wa nje wanavyoviangalia kabla ya kukubali kufanya collabo? – Shetta ana majibu

Collabo za kimataifa ni kitu muhimu kwa mwanamuziki yeyote mwenye malengo ya kujitangaza zaidi nje ya mipaka ya nyumbani. Japo sio kazi rahisi kwa msanii kupata collabo na wasanii wakubwa wa nje kama msanii huyo asipozingatia vitu muhimu.

shetta

Moja ya faida za collabo ni pande zote mbili kupata mashabiki wapya kutoka kila upande wa wasanii hao, ndio maana ni muhimu kwa msanii kujiimarisha kwanza nyumbani na kupata mashabiki wengi, kuongeza namba za followers na kuwa na rekodi nzuri youtube, kwasababu hayo yote yanatoa picha ya ukubwa wa msanii.

mfano ni jinsi collabo ya Vanessa Mdee na K.O ilivyowasaidia wote wawili, Vee imemsaidia kumtangaza zaidi Afrika Kusini na Magharibi, na pia imemsaidia sana kumtambulisha K.O Afrika Mashariki hadi kuamua kufanya media tour mwezi uliopita.

Shetta ambaye kwasasa anajipanga kwa collabo nyingine na msanii wa Nigeria baada ya ile aliyofanya na Kcee, amesema kuwa ili msanii mkubwa wa nje ashawishike kukubali ombi la collabo kuna mambo ambayo mwomba collabo inapaswa ayazingatie.

“unapoomba collabo lazima uambatanishe bio, kama unavyotaka kazi…” alisema Shetta kupitia 255 ya XXL ya Clouds Fm. “lakini kwenye bio unawaambia pia wewe unakuwa mkubwa East Afrika kwasababu mimi ni msanii mkubwa East Afrika… lakini pia wanatakaga kujua unampa nafasi gani nchini kwako au kwenye upande wako wewe unakuwa mkubwa West kupitia mimi, mi napata nini kwako kwahiyo ni lazima umwambie we unaukubwa gani nchini kwako unakotoka na baadhi ya nchi ambazo zimezunguka nchi yako.” Alisema Shetta.

Kwa kauli hiyo ya Shetta ni wazi kwamba kuna haja kwa msanii wa Tanzania kuhakikisha anajijenga vizuri kwanza nyumbani, na kuhakikisha anatengeneza ‘fan-base’ kubwa kabla hajafikiria kuanza kuomba collabo na wasanii wa nje.

Wakati huo huo Shetta amesema kuwa tayari ametuma nyimbo 4 kwa wasanii wa Nigeria, ili wachague ile watakayoikubali kufanya naye collabo. Hiyo itakuwa collabo ya pili ya kimataifa kwa Shetta baada ya ‘Shikorobo’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents