Michezo

Waamuzi wa Angola kuchezesha mechi ya Yanga dhidi ya Rayon Sports

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetaja majina ya waamuzi watakaosimamia mchezo wa Mabingwa watetezi wa ligi kuu Yanga dhidi ya Rayon Sports kutoka Rwanda michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika.

 

Kupitia kwa Mkuu wa Habarai na Mawasiliano wa TFF, Clifford Mario Ndimbo ametaja majina hayo ni Helder Martins Rodrigues De Carvalho (Mwamuzi wa Kati) Ivanildo Meireles De O Sanche Lopes (Mshika Kibendera namba 1), Wilson Valdmiro Ntyamba (Mshika Kibendera namba 2), Joao Amado Muanda Goma (Fourth Official) wote wakitokea Angola.

Wengine ni Abebe Solomon Gibresilassie (Commissioner) (Ethiopia), Yoland Mavouroulou (General Coordinator) (Gabon) na Clifford Mario Ndimbo ( Media Officer) Tanzania.

Mchezo wa Yanga na Rayon hatua ya makundi utapigwa Mei 16 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents