Michezo

Wachezaji wanne ambao ni ‘Target’ ya Man United

Miamba ya soka nchini Uingereza Manchester United inamuwinda kwa udi na uvumba winga wa Borrusia Dortmund, Jadon Sancho, 21 kwenye dirisha la usajili.

Man Utd told age not an issue in Ronaldo return as Berbatov reacts to  transfer talk ยป NBS NEWS
Hata hivyo mashetani hao wekundu wamekusudia kusaini moja kati ya nyota hawa watatu, Ousmane Dembele kutokea Barcelona, Cristiano Ronaldo wa Juventus na nyota wa Chelsea, Hudson-Odoi.

Dembele kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa na Manchester United, ingawaja usajili huo umeonekana kugonga mwamba lakini taarifa zilizopo ni kuwa United hawajakata tamaa.

United pia wamehusishwa na kuhitaji huduma ya Ronaldo, mara kadhaa wameonekana kama wana nia ya kumrudisha Old Trafford nyota huyo baada ya miaka 12 kupita tangu Mreno huyo alipotimkia Real Madrid.

Na wa mwisho ambaye ni tageti ya Mashetani wekundu ni mchezaji wa mabingwa wa Champions League klabu ya Chelsea mchezaji, Hudson-Odoi.

Related Articles

Back to top button