Wafuasi wa TB Joshua wakusanyika kanisani kwake kuomboleza (+ Video)
Wafuasi wa Mhubiri wa Nigeria Temitope Balogun Joshua, maarufu TB Joshua wamekusanyinka katika makao makuu ya kanisa la Synagogue Church of All Nations [SCOAN] mjini Lagos kuomboleza kifo chake.
Kifo cha TB Joshua kilichotokea Jumapili Alfajiri kumeiibua maswali mengi huku baadhi ya watu wakitaka kujua kilitokana na nini.
Kanisa la SCOAN halikuthibitisha chanzo cha kifo cha ghafla cha mhubiri huyo.
Waumini na watu wanaoishi karibu na kanisa hilo walikusanyika kumuomboleza.
“Alikuwa mtu wa Mungu. ISijawahi kuona mhubiri mkarimu anayewasaidia watu hata kama sio wafuasi wa kanisa lake,” Saidat ambaye ni muumini wa dini ya Kiislamu aliiambia BBC.
Nkiru, mmoja wa waombolezaji alisema”Nitamkosa sana. Sijui hili kanisa litaendele vipi baada ya kifo chake.”
Mke wake Evelyn Joshua, mmoja wa wahubiri wakuu wa kanisa la SCOANalielezea kugutushwa na kifo cha ‘’ghafla” cha muwe wake.
“Kumpoteza mwenza sio jambo rahisi; iwe ghafla ua la, inavunja moyo.
“Majonzi huharibu ustawi wetu kwa ujumla. Lakini cha msingi ni kumtumainia Mungu.” Mke wa TB Joshua aliongeza kusema.
“Ni yeye tu [akiashiria Mungu] anaweza kutufariji wakati huu mgumu,” alisema mke wa mhubiri huyo.
Taarifa iliotolewa na kanisa lake la SCOAN siku ya Jumapili alfajiri ilithibitisha TB Joshua alifariki akiwa na umri wa miaka 57.
Bofya hapa chini kutazama.
https://www.instagram.com/tv/CP0BD8Nhzzt/