Habari

Wagonjwa wa kipundupindu wafikia 1,299

IMEELEZWA kuwa hadi kufikia Januari 25, 2024 idadi ya wagonjwa wa kipundupindu nchini wamefikia 1,299 na kati yao 636 bado wanaendelea na matibabu hospitalini.

Hayo yamebainishwa jana na Mhadhiri Msaidizi na mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Theresia Masoi wakati akizungumza na waandishi wa Habari katika mkutano uliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa) kuhusu utengaji wa bajeti ya kujiandaa kupambana na magonjwa ya milipuko ikiwemo Uviko 19 na kipindupindu.

Masoi amesema takwimu zinaonesha kuwa waathirika zaidi wa ugonjwa huo wa kipindupindu ni wanawake na kuongeza kuwa katika takwimu za kidunia inakadiria kuwa kwa mwaka kunakuwa na kesi Milioni 1.3 hadi Milioni 4 huku maeneo ambayo huathiriwa zaidi ni sub-sahara Afrika na Tanzania ikiwa ni mojawapo.

Kwa Upande wake Mchumi Idara ya Sera na Mipango kutoka Wizara ya Afya, Dk. France Lasway amesema mwaka 2023/2024 bajeti ya sekta ya afya inakadiriwa kuwa Sh. Bilioni 2.4 sawa na asilimia nane ya bajeti kuu ya serikali na kwamba kati ya bajeti hiyo wizara inakadiriwa kuwa na kiasi cha Sh. Trilioni 1.2 ambayo ni wastani wa asilimia 7.3 kwa ajili ya kukabiliana na magonjwa ya milipuko.

Amesema wizara imetekeleza afua za kujiandaa na kukabiliana na magonjwa hatari ikiwemo kuhuisha mpango wa dharura ya afya wa kukabiliana na majanga mbalimbali pamoja na kusimamia uanzishwaji wa vituo vitano vya oparesheni ya matukio ya dharura katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha na kufikia idadi ya vituo sit ana kutoa mafunzo kwa wataalamu wa vituo hivyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents