Burudani

Wakazi: SSK isifananishwe na Weusi

Moja ya member wa kundi jipya la Hip Hop nchini ‘Sisi Sio Kundi (SSK),’ Wakazi amesema si vizuri kwa wao kulinganishwa na kundi la Weusi kwa sasa kwani wao wanafanya kitu cha tofauti ingawa wanatambua na kuheshimu uwepo wa wao.

Wakazi

“Weusi ni moja ya magroup yaliyodumu kwa muda mrefu, heshima yao tunawapa lakini watu wasitake kutufananisha au kutulinganisha kwa sababu tunachofanya sisi ni kitu tofauti ingawa tunajua wao wapo na tunaheshimu kuwepo kwao, kwani uwepo wao unatupa sisi maisha na kuna maanisha kuwa magroup bado yapo,

“Moja ya sababu SSK kuanzishwa ni kwamba issue ya magroup ilikuwa kama inakufa hasa magroup ya Hip Hop, so hivyo vitu tukaviweka wazi sasa kukawa na watu wanadis kuwa hatuwezi kufanya vizuri au tufanye vipi ili tuweze kulinganishwa na wengine lakini sisi malengo yetu ni tofauti na vile watu wanavyotaka,” alisema Wakazi.

SSK

Rapa huyo aliongeza kuwa muda mwingine mashabiki wanakuwa na ya kwao kichwani, hivyo wanakuwa wanafikiria wewe ndio unataka uende huko kama wao wanavyoona.

“So hizo ndio issue zilizokuwa zimejitokeza kipindi kile kuhusiana na masuala ya makundi lakini makundi tunayaheshimu yote ya zamani, ya sasa na yanayoibukia ndio washindani wetu. Kundi kama OMG ni washindani kwa sababu tunagombania kinyanganyiro cha kundi bora la Hip Hip, kwanzia Weusi, OMG, TMK hata Chege na Temba still ni group,” alisema Wakazi na kuongeza.

“Lakini tunachokifanya sisi tunasema ni zaidi ya kundi kwa sababu tunataka tujiweke katika nafasi ambayo jamii ituone tuna thamani kubwa zaidi ya sisi kuwa wanamuziki kwao,” alisema Wakazi.

Kundi la SSK linaundwa na Wakazi, P The Mc, Zaiidi na prodyuza Cjamoker kutoka Chimbo Inc.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents