Burudani

Wakenya amkeni ‘muwasupport’ wasanii wenu

Mkataa kwao ni mtumwa. Huu ni msemo unaotumika mara nyingi ili kuwafanya watu kuwa wazalendo na kuthamini vitu vyao zaidi kwa manufaa ya taifa lao.
page

Msemo huo unaendana sambamba na jinsi baadhi ya Wakenya wanavyoshindwa kuwasupport wasanii wao wa muziki ingawa wanafanya muziki mzuri na wakuvutia. Sio tu kusupport nyimbo pamoja na video, bali hata kwenye tuzo mbalimbali za kimataifa ambazo wasanii wao wamekuwa nominated.

Tumeshuhudia wasanii kama Victoria Kimani, Sauti Sol, King Kaka na wengine wengi wakilalamikia kukosa support kutoka kwa mashabiki wao.

“Lupita had to travel and be uplifted by others for you be proud. We are the least patriotic people on this continent as it pertains to the arts. The least supportive …. Kenyans make it hard for an artist to be an artist , this includes fashion art music acting whatever.Then get angry when we are appreciated elsewhere, this is heartbreak,” Hiyo ni kauli ya Victoria Kimani akiwalaumu Wakenya kwa kushindwa kuwasupport wasanii wao lakini kauli hiyo ilitafsiriwa vibaya na Wakenya na kuanza
kushambuliwa.

Hivi karibuni tumeona kazi mpya kama Unconditionally Bae ya Sauti Sol ft Alikiba, Bonbon ya Amani ft Washington pamoja na Give It To Me ya Akothee ft Mr.Flavour. Zote ni kali lakini huenda zisifike popote kutokana na kushindwa kusapotiwa na wazawa.

Tanzania, Kenya na Uganda sote ni ndugu, sina nia ya kupuuza kile kinachofanywa na baadhi ya mashabaki katika kusupport wasanii wao, lakini juhudi iongezeke ili kuwatia moyo wasanii wenu ambao wengi wao wapo katika hatua ya kukata tamaa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents