Habari

Wakonta akabidhiwa bahasha la mamilioni hadharani, Rais Magufuli ampa maneno ya faraja (+video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.  John Pombe Magufuli amemzawadia kitita cha tsh milioni 10  mwandishi wa scripts za filamu nchini , Wakonta Kapunda  kwa lengo la kumuunga mkono katikakazi yake licha ya kuwa ni mlemavu.

Rais Magufuli ametoa zawadi hiyo leo Jumatatu Julai 2, 2018 katika uzinduzi wa kitabu cha Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi kinachoitwa, ‘I CAN, I MUST, I WILL’.

Wakonta amepewa fedha hizo baada ya kujinyakulia kitita cha Dola $20,000 za Marekani sawa na Sh45.6 milioni, ikiwa ni zawadi ya ushindi wa shindano la kuandika wazo la kibiashara lililotolewa na Dk Mengi.

Rais Magufuli amesema kuwa “nilisoma kwamba aligongwa na gari siku ya mahafari yake, lakini hajakata tamaa hana uwezo wa kuandika kupitia mikono yake, lakini anaweza kuandika anachokifikiria kwa kutumia ulimi wake, nitamchangia Sh10 milioni iweze kumsaidia katika mawazo yake anayoyapata.

Tazama video Magufuli akiongea kuhusu zawadi hiyo.

Wakonta kwa sasa ni mlemavu wa kupooza na amekuwa akiandika kwenye simu yake kwa kutumia ulimi hii ni baada ya kupata ajali ya gari.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents