Habari

Wanafunzi wakalia ndoo za maji, vigoda darasani

Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mkwawa iliyopo katika kijiji cha Iringa Mvumi, Wilaya ya Chamwino, mkoani Dodoma, wanalazimika kukalia ndoo za maji, madumu na vigoda.

Na Mary Edward, PST Dodoma

 
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mkwawa iliyopo katika kijiji cha Iringa Mvumi, Wilaya ya Chamwino, mkoani Dodoma, wanalazimika kukalia ndoo za maji, madumu na vigoda.

 

Hali hiyo imetokana na uongozi wa kijiji hicho kudaiwa `kutafuna` Sh. milioni 21 fedha za michango ya wananchi ambazo zingewezesha ununuzi wa madawati na ukarabati wa jengo wanalosomea wanafunzi hao.

 

PST ambayo ilitembelea shule hiyo, ilishuhudia baadhi ya wanafunzi kukalia ndoo za plastiki, madumu na wengine vigoda.

 

Ni madawati 10 tu yaliyokutwa katika moja ya darasa la shule hiyo.

 

Akizungumza na PST, Mkuu wa Shule hiyo, Bw. Samweli Chimosa, alisema hali hiyo imetokana na wazazi na walezi katika kata hiyo, kugoma kuchangia fedha za kununulia madawati kufuatia uongozi wa kijiji cha Iringa Mvumi, kushindwa kuwaeleza wananchi matumizi ya Sh. milioni 21, walizochanga kwa ajili ya ukarabati wa jengo la shule.

 

“Hali hii unayoiona ni matokeo ya Sh. milioni 21 kutojulikana zilipo ambazo zilitakiwa kukarabatiwa jengo hili la ofisi, na zingine zingebaki zingetumika kwa ajili ya kuchonga madawati ya wanafunzi,“ alisema.

 

Hata hivyo, Mkuu huyo wa shule aliwaomba wazazi na walezi, kuwaonea huruma watoto wao, na badala yake wasahau yaliyopita ili wawawekee mazingira mazuri ya kusoma, ambayo yatawafanya wapende shule na kufaulu vizuri.

 

“Nawasihi wazazi, waache kususia kutoa michango,.. watoto hawa ni wao ,�wanaopata shida ni watoto na sio hao viongozi, hivyo wito wangu waendelea kuchangia elimu, ili watoto wao wasome katika mazingira mazuri’alisisitiza.

 

Aliongeza kwamba, shule hiyo yenye jumla ya watoto 121 inayohudumia vijiji vya Ikombolinga na Iringa Mvumi katika Kata Iringa Mvumi yenye kidato cha kwanza na pili, ni wanafunzi 40 tu ndiyo wanaokalia madawati.

 

Bw. Chimosa aliyataja matatizo mengine yanayoikabili shule hiyo ni pamoja ukosefu wa meza za walimu ambao wanalazimika kutumia madawati na madirisha ya jengo hilo ambayo mpaka sasa hayajakamilika vizuri.

 

Alisema kuwa, pamoja na kuwashawishi wazazi na walezi juu ya michango yao, lakini imeshindikana kutokana na hasira waliyonayo juu ya fedha zao.

 

 

 

Source: Nipashe

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents