Habari

Washinda Mlimani na Mbunge wao kisa Maji (+Video)

Januari 7, 2020 Mbunge wa Makete ameshirikiana na Wananchi wa Mang’oto vijiji vyote kufanya kazi ya maendeleo kwa kusafisha Intake ya Maji iliyopo kwenye milima umbali wa KM 7 hadi 8 kutokea kijiji cha Malembuli.

Ni masaa 2 yametumika kupanda mlima huo na baadae kufika eneo lililotegwa Maji ambalo takribani wiki nzima limeziba na kusababisha ukosekanifu wa Maji kwa Wananchi wa Mang’oto.

Sanga ambaye ameshirikiana na wananchi hao kusafisha intake amesema ” nawashukuru wananchi kwa kujitokeza kwa wingi, nimepanda mlima huu kwa tabuu kweli na sehemu zingine ilinibidi niweke vituo vya kupumzika hadi nimefika, Furaha yangu ni kujumuika nanyi kwenye kazi hii ambayo kwa leo imeleta matumaini ya kupatikana kwa Maji, nawashukuru kwa uchaguzi, mmetuamini tushirikiane kwenye kuchapa kazi”

Sanga anafika Mang’oto kwa mara pili ndani ya wiki moja ambapo siku chache zilizopita alikwenda kijiji cha Ilindiwe kufunga Solar ya Umeme kwenye Zahanati ili huduma za Afya zitolewe wakati wote usiku na mchana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents