Bizzare

Watu 366 wametangaza nia kugombea urais wa Marekani hadi sasa, unashangaa Tanzania?

Viongozi wa chama tawala nchini, CCM wanaendelea kujitokeza kwa wingi kutangaza nia ya kuwania urais kwenye uchaguzi mkuu, 2015.

dd
Mamia ya watu wamejaza fomu ya kuwania urais wa Marekabni mwaka 2016. Watu hao wanatoka kwenye kila aina ya makundi. Hawa kwenye picha ni miongoni mwao

Wingi wa watangaza nia hao nchini Tanzania umeonekana kuwa mkubwa zaidi kuwahi kuonekana. Lakini hiyo ni kama tone kwenye ndoo ya maji ukilinganisha na watu waliotangaza nia ya kugombea urais wa nchini Marekani mwakani.

Hadi sasa ni watu 366 ambao tayari wamejaza fomu za tume ya uchaguzi ya nchini humo kuweka wazi nia zao. Orodha hiyo bado inazidi kuongezeka.

Hata hivyo baadhi ya wagombea wanachekesha kiasi. Kwa mfano Thomas Keister anataka kuwania kupitia chama chake, Marijuana Party.

Mwingine ni Princess Khadijah M. Jacob-Fambro wa Revolutionary Party kutoka California ambaye kwenye sehemu anayotakiwa kutaja jina la kamati yake ya kampeni aliitumia kutoa ofa kwa Lil Wayne ili awe mume wake.

Ni rahisi sana kwa Marekani kutangaza nia ya kugombea urais. Anachohitaji mgombea ni kuwa na muda tu wa kujaza fomu za F.E.C. (tume ya uchaguzi) na kwakuwa zinapatikana kwenye mtandao na haina hata haja ya kutuma kwa njia ya posta.

Kwa Marekani raia yeyote mwenye zaidi ya miaka 35 anaweza kugombea urais.

Chanzo: New York Times

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents