Michezo

Wayne Rooney ashushiwa ‘rungu zito’ na mahakama

Mshambuliaji wa klabu ya Everton, Wayne Rooney leo amepigwa marufuku na mahakama ya kutokuendesha gari kwa miaka miwili na adhabu ya kusaidia kazi za jamii ikiwemo usafi kwa masaa 100 .

Wayne Rooney katikati kwenye picha.

Adhabu hiyo imekuja baada ya mshambuliaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya England, kukamatwa akiendesha gari akiwa amelewa mapema mwa mwezi huu huko Cheshire nchini Uingereza.

Hata hivyo tayari Wayne Rooney amekubali adhabu hiyo ya mahakama na kuwaomba radhi mashabiki wa klabu ya Everton na familia yake.

Kufuatia hukumu ya mahakama napenda niiombe radhi familia yangu, kocha wangu na uongozi wa Everton na kila shabiki wa Everton na watu wote wanaonisapoti

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents