Habari

Waziri Kairuki awashushia rungu Maafisa utumishi

Serikali kupitia Waziri wa nchi ofisi ya Rais Utumishi na Utawala bora Angella Kairuki ametangaza kwa maofisa utumishi wote ambao watachelewesha mishahara baada ya mtumishi kupandishwa daraja watafungiwa mishahara yao ili na wao waweze kupata uchungu.

Akizungumza leo Bungeni Mjini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza na Mbunge wa Karagwe, Innocent Bashungwa,

“kuna changamoto ya wale watumishi waliopandishwa madaraja mishahara huwa inachelewa kureflect lile daraja ambalo wamepandishwa. Je, ni nini maelezo ya serikali kuhusu hilo.”

“Tulishachukua katika halmashauri ya Bagamoyo na Kinondoni pia Hatuta mvumilia Afisa Utumishi yoyote au muhusika yoyote katika mamlaka ya ajira ambaye atachelewesha malipo ya mshahara baada ya mtumishi kupandishwa daraja,” alisema Waziri Kairuki.

“Nipende tu kusema sasa hivi tumeenda mbali tutafika wakati tutaanza hata kuwafungia Wakurugenzi wa halmashauri mishahara yao ili waweze kuona uchungu wa kuchelewesha kupandishiwa,” ameongeza Waziri huyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents