Michezo

Wenger: Nimechoshwa na beef ya Mourinho

Boss wa klabu ya Arsenal, Mzee Arsene Wenger amesema yupo tayari kuelewana na Meneja wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho. Mokocha hawa wawili wamekuwa na hali ya kutokuelewana kwa zaidi ya mwaka sasa.

Wenger bado anasubiri Mourinho ashinde katika michuano ya Europa ili wapate kurudisha amani iliyopotea kati yao. Wawili hawa walizungumziwa katika vyombo vya habari mbali mbali kutokana na tofauti zao tangu enzi akiwa Meneja wa klabu ya Chelsea mwaka 2014.

Wenger ameahidi kuyazungumzia hayo katika kikao chake kijacho, huku kocha huyo akionekana kana kwamba zama zake za kuwepo klabuni hapo kunamalizika baada ya kuzuka kwa maandamano ya mashabiki wa klabu hiyo kumtaka kuondoka. Wenger amekua kwenye club ya Arsenal kwa zaidi ya miaka 20.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents