Michezo

yanga yaweka rekodi ya kutisha Klabu Bingwa Afrika

Michuano ya klabu Bingwa Afrika inaendelea huku timu mbalimbali zikiwa zinaweka rekodi zao tofauti tofauti moja wapo ya timu ambayo imeweka rekodi mbalimbali ikiweko ni mara ya kwanza toka kuanzishwa kwa Klabu ya Yanga kufuzu kuelekea hatua ya robo fainali ila rekodi inayowafurahisha na kuwachanganya mashabiki na viongozi wa Yanga ni kuwa klabu pekee inayoongoza kwa upachikaji wa mabao pamoja na ugeni wao kwenye michuano hiyo.

Mpaka sasa Yanga imeshafuzu hatua ya robo fainali huku ikiwa ni timu inayowatishia vigogo wengi kukutana nayo kwa aina ya mpira unaochezwa na timu ya Yanga wachezaji wanaonekana kuwa na morali ya juu mno katika michezo.

Hii maana yake Yanga kwa sasa imeanza kuwa tishio Afrika vigogo wengi wameanza kuifuatilia timu kwa ukaribu sana, Yanga uwekezaji wake ndio umeifanya mpaka kuwa hivi ilivyo uwekezaji wa GSM nguvu inayotumiwa na Injinia Hersi Saidi kuhakikisha analeta wachezaji bora, ushirikiano kati ya viongozi kwa viongozi pamoja na umoja wa wanachama pamoja na mashabiki ndio silaha pekee ya matokeo haya yanayoendelea.

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents