Burudani

Young Killa, Roma, Temba waahidi makubwa Serengeti Fiesta Shinyanga

Baada ya kutarajiwa kutoa burudani ya nguvu kwa wakazi wa Musoma kwenye tamasha la Serengeti Fiesta katika Uwanja wa Karume Ijumaa hii, wakali wa burudani wa tamasha hilo sasa wamekita kambi katika mkoa wa Shinyanga ikiwa na lengo la kutoa burudani ya nguvu kwa wakazi wa mji huo Jumamosi.

Young Killer Msodoki akiwa kwenye hisia

Young Killa, Roma na Temba wakisindikizwa na wazanii wengine zaidi ya nene wameahidi kufanya makubwa katika tamasha hilo litakalofanyika katika uwanja wa Kambarage mjini humo. “Ahadi yetu ni moja tu, burudani ya nguvu…mashabiki zangu wajiandae, waje kwa wingi uwanjani tuburudike pamoja,“ alisema Young Killa.

Msanii huyo ambaye ni kati ya wasanii wadogo Tanzania amekuwa kipenzi cha wengi hasa kutokana na umahiri wake katika kuimba. Kwa sasa mwanamziki huyo anatamba na vibao kama Umebadilika, nahitaji maadui na vingine vingi.

Mh. Temba na Roma hawakusita kutoa yao ya moyoni, “tumejipanga kutoa burudani ambayo wamekuwa wakiisubiri kwa hamu sana. Uzoefu tulioupata katika majukwaa ya mikoa mingine utatumika ipasavyo ili kuhakikisha tunagawa dozi ya nguvu,” walisema wanamuziki hao.

Akiongea na mwandishi wetu, Meneja wa bia ya Serengeti, Rugambo Rodney alisema kwamba yakiwa yamebaki masaa kadhaa kabla ya Serengeti fiesta kutua Shinyanga, ununuzi wa tiketi umekuwa ni wa kudhirisha sana. “Wauzaji wa tiketi katika vituo vyetu mbalimbali wamekuwa wakitupa taarifa kwamba ununuzi wa tiketi ni wa kuridhishja sana,” alisema. “Kwa mtazamo wa kadiri, inatudhihirishia kwamba wamejiandaa kuipokea Serengeti fiesta kwa hamu, na kwa upande wetu tunawahakikishia burudani ya nguvu,” aliongeza Rodney.

Wasanii wanaotarajiwa kupanda jukwaani ni pamoja na Stamina, Nay wa Mitego, Roma Mkatoliki, Christian Bella, Chege, Mhe Temba, Young Killer, Shilole, Nick wa II, Recho na Barnaba huku wakisindikizwa na wasanii chipukizi wa maeneo mbalimbali ya Shinyanga na vitongoji vyake.

Tamasha hilo la Serengeti Fiesta pia litaambatana na shughuli mbalimbali za burudani kama vile Serengeti Soka Bonanza na shindano la dansi la Serengeti Fiesta, na kumtafuta Serengeti Super Nyota Diva’s.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents