Michezo

Zahera ajitetea kuhusu kuvaa Kipensi ”Prince Henry wa Uingereza anavaa hivi, Kukosa heshima ni kuidharau Yanga” (+video)

Kocha wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera amejitetea kuhusu kuvaa kipensi hadi kupelekea kupigwa faini na TFF ya Tsh 500,000.

Image result for mwinyi zahera

”Wanasema namna ambavyo mimi navaa, ni kukosa heshima. Nakosea wapi heshima ?,Prince wa Monaco, Prince Henry wa Uingereza wanavaa hivi. Kukosea watu heshima ni kuidharau Yanga SC.”

”Timu kubwa kama Yanga mnaizarau, mnaiyonea huko ndiyo kukosa heshima, sio kuvaa hivi ndiyo kukosa heshima.” – Amemalizia Zahera.

Kwa upande wa adhabu ya kufungiwa mechi tatu amesema ”Kocha msaidizi yupo pale anajua ‘Philosophy’ ya kocha, yatakayotokea uwanjani kwa mchezaji anajua chakufanya.”

Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ametozwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kuvaa mavazi yasiyo nadhifu na ya heshima katika mechi namba 9- Yanga 0 vs Ruvu Shooting 1, kinyume na Kanuni ya 14(2m) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo. Adhabu dhidi yake imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 41(13) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Makocha.

https://www.instagram.com/p/B2AFv-cADXS/

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents