Uncategorized

Zahera awapa ofa ya chakula waandishi wa habari, kuhusu Mapinduzi Cup adai wataangalia wapi kunafaida

Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera amewapa ofa ya chakula cha mchana waandishi wote wa habari za michezo waliyohudhuria kwenye kikao chake.

Kocha Zahera mbali na yote aliyozungumza kwenye mkutano amesema waandishi wa habari za michezo Tanzania nimoja ya watu waliofanya naye kazi vizuri kwa mwaka 2018.

“Leo ni siku ya mwisho ya mwaka 2018 kwasababu hiyo naomba kushukuru watu wote waliofanya kazi nasisi vizuri kama Yanga mkiwemo waandishi wa habari,’’ amesema Zahera.

Mwinyi Zahera ameongeza “Tunaenda kuanza mwaka 2019 kamaYanga tukiwa tunaongoza ligi yote hii ni kwasababu ya wachezaji wangu ambao licha ya matatizo yote tuliyonayo wao wameyageuza kuwa furaha kwao na kuwapa furaha mashabiki. Kwa kuendelea kushinda mechi zetu mpaka sasa tumeshinda 16 nawashukusru sana wachezaji wangu.’’

Kwa upande wa mashindano ya Kombe la Mapinduzi Zahera amesema “Kufuatana na nguvu yetu tulionayo (wachezaji) inatubidi tuangalie wapi tutapata faida, tupo na ligi kuu, tupo na Azam federation cup, mapinduzi Cup na Sport Pesa inabidi sisi kama Yanga tuwe na malengo kwenye kitu chenyemanufaa kwetu tukiamua kuyataka makombe yote tunaweza kosa yote hivyo lazima baadhi ya wachezaji wapumzike kwaajili ya ligi na ASFC.”

“Salamu zangu zingine za mwaka mpya ziende kwa mashabikiwa Yanga, hawa watu ni hatari sana tunawashukuru sana. wako nasisi kila sehemu.’’

Yanga wanamaliza mwaka huu wa 2018 huku wakiongoza ligi kuu soka Tanzania Bara kwa kuwa na jumla ya pointi 50 wakicheza michezo 18.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents