AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Aaron Ramsey kumfuata Ronaldo Juventus, vipimo vya afya kufanyika wikiendi hii

Kiungo wa klabu ya Arsenal, Aaron Ramsey amekubali kujiunga na Juventus.

Ramsey ataondoka Arsenal kama mchezaji huru wakati ambapo mkataba wake utakapo fikia kikomo mwishoni mwa msimu huku ikiliezwa kuwa kujiunga kwake na Juve ni chaguo lake binafsi.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales, atakwenda Juventus kufanyiwa vipimo vya afya siku ya Jumapili na dili hilo kuwekwa hadharani mara baada ya mchezo wa Italian Super Cup dhidi ya AC Milan Jumatano ijayo.

Tangu Januari 1, kiungo huyo amekataa kuingia kandarasi mpya dhidi ya The Gunners huku akiwa na nafasi ya kujiunga na klabu yoyote nje ya Uingereza.

Ramsey amejiunga na Arsenal akitokea Cardiff mwaka 2008 na kufanikiwa kufunga jumla ya mabao 52 kwenye michezo 252 ya Premier League aliyocheza.

Mshindi huyo mara tatu wa FA Cup akiwa na the Gunners, Ramsey alitupia bao la ushindi kwenye fainali yao dhidi ya Hull mwaka 2014 na Chelsea 2017.

Kwa sasa anakwenda kuungana na Cristiano Ronaldo kwenye moja ya klabu kubwa barani Ulaya ya Juve.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW