Burudani

Anachojivunia msanii wa Norway ‘Makihiyo’ kutoka kwa Ben Pol (+video)

Msanii muziki kutoka nchini Norway,  Makio amefunguka jinsi ngoma ‘Ni Wako’ ambao aliyomshirikisha Ben Pol ilivyofanya mazuri.

Muimbaji huyo ameimbia Bongo5 kuwa mapokezi ya ngoma hiyo yamekuwa makubwa si kwa Bongo tu bali hata nchini kwao.

“Mapokezi ni mazuri watu wamependa wimbo na wamefurahi sana na ninaimba Kiswahili na ninafanya style ya Bongo flava, na sikujua kama watapokea vipi kwa sababu ilikuwa style mpya kwa mimi kuimba lakini watu wamependa nimefurahi sana,” amesema Makihiyo.

Alipoulizwa mapokezi kwa upande wa Norway yapo vipi, alijibu: “Watu wanaipenda pia sana off course wahajui kiswahi lakini bado wanaipenda na kulikuwa na watu sijaongea nao miaka mingi sana wananiandikia kunipongeza”.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents