Uncategorized

Anthony Martial afuta ghafla account zake za mitandao ya kijamii, mashabiki wahofia kutimka Man United

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United, Anthony Martial ghafla ameamua kufutilia mbali mitandao yake ya kijamii bila kutoa sababu za yeye kufanya maamuzi hayo.

Watu mbalimbali wakiwemo mashabiki zake waliyomfuatilia kwenye kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram wamekuwa wakikutana na ujumbe unaosema “Sorry, this pageisn’t available. The link you followed may be broken, or the page may have beenremoved. Go back to Instagram.”

Alkadhalika hata kwenye mtandao wake wa kijamii wa Twitter kupitia @AnthonyMartial hivyo kuzua utata hasa kwa mashabiki kutokana na utamaduni wake kwani mwezi Mei mwaka jana alifuta picha zake nyingi na kusababisha wengi kudhania kuwa nyota huyo yupo mbioni kutimka Old Trafford.

Mbali na tukio lake hilomchezaji huyo wa taifa wa Ufaransa ameifungia Manchester jumla ya mabao tisaambayo sawa na aliyoweka kambani kiungo wa timu hiyo PaulPogba.

Mkataba wa Martial ndani ya United utafikia tamati mwishoni mwa msimu jao huku kocha Solskjaer  kabla ya mechi na Bournemouth siku ya Jumapili amesema kuwa anaimani ataweza kumshawishi  nyota huyo kuongeza kandarasi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents