Tupo Nawe

AS Roma yawazuia wachezaji wake kupiga picha na Drake, kila mwanasoka aliyefanya hivyo timu yake huambulia kipigo

Miamba ya soka nchini Italia klabu ya AS Roma imetangaza kuwafungia wachezaji wake kupiga picha na msanii maarufu wa muzi wa Marekani, Drake.

Roma imewataka wachezaji wake kutopiga picha na msanii huyo hadi mwishoni mwa msimu utakapomalizika huku wakishindwa kutoa sababu.

Taarifa zilizopo kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii zinaeleza kuwa wachezaji wote waliopiga picha na Drake wamekuwa wakipata matokeo mabovu ya kufungwa kwenye mechi zao zinazofuata mara baada ya tukio hilo la picha.

Aprili 13 inadaiwa mchezaji wa PSG, Layvin Kurzawa alipiga picha na Drake na kuiweka kwenye akaunti yake ya Instagram na timu yake kupokea kichapo cha mabao 5 – 1 dhidi ya Lille siku ya Jumapili.

Mshambuliaji wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang ni miongoni mwa wahanga hao baada ya kupiga picha na rapper huyo mwenye asili ya Canada Aprili 2 huku wakishika jezi ya Arsenal siku iliyofuata Jumapili klabu hiyo iliambulia kipigo cha bao 1 – 0 dhidi ya Everton kwenye dimba la Goodison Park .

Pierre-Emerick Aubameyang (left) gave Drake his Arsenal shirt after his gig at the O2 in April

Paul Pogba pia alikuta na staa huyo na kupata kupiga picha na Drake na kujikuta Manchester ikishindwa kafanya vizuri kwenye mechi zake zilizofuata.

Paul Pogba (left) poses for a picture with Drake (right) after his gig in Manchester in March

Akiwa na kikosi cha Ole Gunnar Solskjaer Pogba alishuhudia akiona jahazi linazama mara baada ya kutolewa FA Cup na Wolves.


Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW