Siasa

Balali Kwisha kazi!

Kama kuna watu waliocheza lile dili la kuchota mapesa ya Benki Kuu ya Tanzania, BoT kupitia ile akaunti ya madeni ya nje, EPA, ambao wamejichimbia majuu wakidhani wataepuka mkono wa dola, wajihesabu wamekwisha!

Na Mwandishi Wa Alasiri, Jijini

 

 

 
Kama kuna watu waliocheza lile dili la kuchota mapesa ya Benki Kuu ya Tanzania, BoT kupitia ile akaunti ya madeni ya nje, EPA, ambao wamejichimbia majuu wakidhani wataepuka mkono wa dola, wajihesabu wamekwisha!

 

 

 

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema amesema piga ua galagaza watu wote waliohusika na dili hilo haramu, hata wawe wamejichimbia kona gani duniani, watadakwa na kufikishwa kwenye mkono wa sheria.

 

 

 

Amesema makachero wa Kibongo na wale wa kimataifa almaarufu kama Interpol, watasaidiana kufanikisha zoezi hilo la kuhakikisha hakuna fisadi anayeponyoka.

 

 

 

Kwa mtaji huo, aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dk. Daudi Balali, na ambaye alikuwa mtu wa kwanza kutuhumiwa kushiriki dili hilo, ajihesabu amekwisha, kwani kama uchunguzi utabaini alihusika, makachero watamdaka juu kwa juu na kumrejesha Bongo kukabiliana na kesi.

 

 

 

Kutokana na uchunguzi huo kuanza miezi miwili iliyopita, kuna uwezekano mkubwa hivi sasa makachero wa Kitasha wakawa wameanza kumlia mingo ili kubaini uhusika wake katika dili hilo lililolipotezea taifa mabilioni ya pesa.

 

 

 

Hivi sasa, kuna taarifa tofauti zinazodai kuwa Dk. Balali amejichimbia katika visiwa vya Malta, wengine wakidai yuko Boston Marekani na baadhi wakidai kuwa hajulikani aliko.

 

 

 

Source: Alasiri

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents