Habari

TMH wafungua kituo cha watoto yatima

TMHHivi karibuni shirika lisilo la kiserikari Tanzania Mitindo House limezindua kituo kipya cha kulelea watoto yatima na walioathrika na janga hatari la ukimwi, ikiwa ni moja ya maazimio ya shirika hili lililoundwa na wanamitindo maarufu hapa nchini.

TMH

 

 

 

Hivi karibuni shirika lisilo la kiserikari Tanzania Mitindo House limezindua kituo kipya cha kulelea watoto yatima na walioathrika na janga hatari la ukimwi, ikiwa ni moja ya maazimio ya shirika hili lililoundwa na wanamitindo maarufu hapa nchini.

 

 

 

Uzinduzi ulifanyika katika nyumba moja ambayo waliikodisha kwa lengo maalum kwa ajili ya kuwapa hifadhi watoto hao, iliyopo maeneo ya magomeni mikumi mtaa wa kisiju nyumba namba tisa, unaweza kuona ni hatua kubwa ambayo wamefikia katika kuhakikisha usalama wa watoto hawa ambao walikosa malezi.

 

TMH

 

“unajua kila mtu anakuwa na lake la kusema eti sisi tunafanya haya yote kwa maslahi yetu binafsi jambo ambalo sio la ukweli kabisa kwani kila tunachokifanya kimekuwa kikionekana dhahiri na pia tumekuwa tukisisitiza sana watu walete misaada ya vitu zaidi sasa ikiwa utaletewa magunia ya mchele ina maana tunayauza au? Alisema Bi Khadija Mwanamboka akiwa kama Mwenyekiti na Afisa mahusiano wa shirika hilo.

 

 

 

Shughuli hiyo ilihudhuriwa na watu mbali mbali wakiwemo watoto ambao walijitokeza kuja kuwapa sapot watoto wenzao, pia kulifanyika mnada ambao uliweza kuingiza kiasi cha fedha, halikadhalika mgeni rasmi alikuwa ni Mbunge wa wilaya ya Same Bi Anna Kilango Malecela ambaye alikabidhi vitu mbali mbali kwa watoto hao kama vile dawa za mswaki, maziwa, sabuni n.k

 

 

 

Kwa kweli Tanzania Mitindo House inastahili pongezi kwa yote ambayo wameyafanya katika kipindi kifupi tangu kuanzishwa kwa shirika hilo.

 

 

 

Uanweza kupata ujumbe fupi kutoka kwa bi Khadija Mwanamboka kwa kupitia video hapa chini:

 

 

 

{denvideo http://www.bongofive.com/kideo/videos/khadija_kituo.flv}

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents