Promotion

Benki ya NMB yazindua Chap Chap akaunti kwaajili ya Watanzania wasio na akaunti

Benki ya NMB imeendelea kuwa kinara katika kubuni na kuboresha huduma mbali mbali za kibenki, ili kuwawezesha wateja wake kupata unafuu na urahisi wa upatikanaji wa huduma za kibenki nchini Tanzania.

NMB Mgimwa (640x520)
Mheshimiwa waziri wa fedha Dk William Mgimwa akichukuliwa alama za vidole na Ofisa mauzo ya Nje NMB Abdul Kandoro mara baada ya uzinduzi rasmi wa NMB chap chap akaunti mwishoni mwa wiki mkoani Dodoma

Katika kulizingatia hili mwishoni mwa wiki Benki ya NMB ilizindua akaunti ya Chap Chap ambayo kusudi kubwa ni kuwafikia wananchi wote kule waliko na kuwafungulia akaunti zao.Kikubwa zaidi ni kwamba mteja ataweza kufungua akaunti papo hapo na kupata kadi yake ya kutolea fedha ndani ya dakika kumi.

• Mambo muhimu zaidi ambayo mteja wa Chap Chap anaweza kufaidika nayo ni pamoja na:
• Kuona salio la akaunti yako popote ulipo
• Kuweka fedha na kutoa fedha kwa mawakala wa M- pesa
• Kutuma fedha kwa wasio na akaunti mahali popote nchini kwa kutumia huduma ya Pesa Fasta
• Kununua vocha za muda wa maongezi kutoka kwenye mtandao wowote wa simu
• Kuchukua fedha hadi shillingi 1.000,000/= kutoka kwenye ATM

IMG_1473 (2)
Ofisa mtendaji mkuu wa benki ya NMB Mark Wiessing akimshukuru mheshimiwa waziri wa fedha Dk William Mgimwa mara baada ya kuzindua akaunti ya NMB Chap chap

IMG_1469 (640x392)
Sehemu ya maofisa na wageni waalikwa kwenye uzinduzi huo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents