Tupo Nawe

Bushoke: Siwezi kuwashirikisha wasanii wapya wanaofanya vizuri ili nirudi kwenye chati

Bushoke amesema kuwa hafikirii kumtumia msanii yeyote mpya anayefanya vizuri kwa sasa kwenye game kama daraja la kurudi kwenye chati.

bushoke

Muimbaji huyo wa ‘Dunia Njia’ ni miongoni mwa wasanii wenye uwezo mkubwa waliofanya vizuri kipindi cha nyuma lakini sasa hawatambi kama zamani.

Bushoke ameiambia Planet Bongo ya East Afrika Radio kuwa endapo atamshirikisha msanii yeyote mpya au wa zamani ni kwasababu ameona anafaa katika ngoma husika kwa muda huo, lakini kamwe haamini kama kumshrikisha msanii anayekiki ni njia nzuri ya kurudi kwenye chati.

Anatarajia kuachia ngoma zake hivi karibuni na amepanga collabo yake ijayo atawashirikisha Mandojo na Domokaya.

Jay Moe pia hivi karibuni alikaririwa akisema kauli kama hii na kuongeza ndiyo sababu hakutaka kumshirikisha msanii anayefanya poa kwenye ngoma ya ‘Hili GameE’ ili isionekane kabebwa wakati uwezo anao.

Credit: dullahplanet (Instagram)

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW