Burudani

Dogo Mfaume wa ‘Kazi Yangu ya Dukani’ kuzikwa Chanika

Msanii wa muziki wa Mchiriku, Mfaume Selemani maarufu kama  Dogo Mfaume aliyefariki Jumatano hii wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN), atazikwa Ijumaa hii Chanika jijini Dar es salaam.

Dogo Mfaume enzi za uhai wake

Akiongea na Bongo5 Alhamisi hii, kwa niaba ya familia Mmiliki wa kituo cha Back To Life Sober House kinachotoa matibabu kwa waathirika wa dawa za kulevya, Pilli Missanah, amedai mwili wa marehemu Dogo Mfaume utachukuliwa Hospitali ya Muhimbili saa mbili asubuhi na kuupeleka Chanika kwa ajili wa mazishi.

“Tunamshukuru mungu mambo yanaenda vizuri, mwili wa marehemu utachukuliwa Muhimbili saa mbili asubuhi kwaajili ya mazishi saa saba mchana, Chanika kwa Mbiki jijini Dar es salaam. Kwa mtu ambaye anataka kuja atapanda gari za Gongolambo halafu atashuka Gongolambo baada ya hapo atapanda gari la Chanika atashuka kwa Mbiki,” alisema Pilli Misana.

Alisema kwa yoyote ambaye ameguswa  na msiba huo anaweza kuwasiliana na kaka wa marehemu, Selemani kupitia namba 0718005138.

Kifo cha muimbaji huyo kimekuja ikiwa ni siku chache tangu Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamisi Kigwangalla kutoa msaada kwa ajili ya matibabu ya uvimbe karibu na ubongo uliokuwa unamsumbua.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents