Uncategorized

Everton yaivuruga Manchester United, hatma ya De Gea, Pogba na Lukaku inategemea ‘Top Four’

Wachezaji bora kabisa ndani ya Old Trafford, David de Gea, Paul Pogba na Romelu Lukaku wanatarajiwa kuthibitisha kuendelea kubaki ndani ya klabu hiyo endapo United itasalia kwenye nafasi nne za juu ‘Top Four’ msimamo wa Premier League ambao utawawezesha kushiriki Champions League.

Hali hii tata ya wachezaji hao kuanza kuonyesha kutafuta mlango wa kutokea imekuja mara baada ya United kukubali kipigo cha mabao 4 – 0 kutoka kwa Everton siku ya Jumapili na hivyo kuwaweka kwenye nafasi ngumu ya kuingia ‘Top Four’ ya msimamo wa ligi ili kushiriki Champions League msimu ujao.

Mpaka hivi sasa, De Gea hajakubaliana na United juu ya mkataba wake mpya ambao umesalia mwaka mmoja ukitarajiwa kumalizika ifikapo mwaka 2020. Endapo timu hiyo itamaliza nje ya nne bora itakuwa ngumu kwa mlindalango huyo kubaki kwenye klabu hiyo.

Pogba ambaye amesajiliwa akitokea kwenye klabu ya Juventus mwezi Agosti mwaka 2016 kwa mkataba wa miaka mitano, amekuwa akihitaji na Barcelona hali iliyopelekea wengi kuamini angeondoka kipindi cha kiangazi kwa matokeo ya juzi yanawafanya watu kufikiria kuwa wachezaji hao wameshindwa kuipa heshima timu hiyo.

Alipoongea mara baada ya mchezo wa hapo juzi dhidi ya Everton, Pogba amesema “Kwa namna tulivyocheza, na uwezo tulioonyesha kama timu, na kila mmoja wetu ni kuivunjia heshima.”

“Tumeshindwa kujiheshimu hata sisi wenyewe, mashabiki wetu na mashabiki pia. Kila kitu kimekwenda hovyo.”

Lukaku mwenye umri wa miaka 26 mkataba wake unamalizika mwaka 2021, ameshindwa kuwa kwenye kikosi kinachoanza chini, Solskjær ukijumlisha na kama watashindwa kushiriki Champions League bila shaka hatoweza kubaki.

Kwa kushindwa kupata ushindi mbele ya Everton kumetokana na United kupiga shuti moja pekee lililolenga lango jambo lililopelekea aliyekuwa kocha wa klabu hiyo José Mourinho kuwa kwenye hali mbaya na kutimuwa mwishoni mwa mwezi Desemba na nafasi yake kuchukuliwa na Solskjær.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents