Bongo MovieBongo5 ExclusivesVideos

Exclusive Videos: Cloud 112 amkaribisha baby boy wake Nabil aka Cloud Junior

[youtube]http://www.youtube.com/watch?v=NeJNxMVDXLI[/youtube] Mwigizaji Issa Mussa maarufu kama Cloud 112 siku ya wanawake duniani alishangilia kwa mtindo wa kipekee baada ya mkewe Cynthia kujifungua mtoto wa kiume. Mkewe huyo ambaye pia ni msanii mwenzake, alijifungua kwa njia ya upasuaji katika hospitali ya Aga Khan muda wa usiku.

Cloud anasema mwanaye anatarajia atakuwa muigizaji mzuri na mwenye baraka hasa baada ya kuzaliwa siku ya alhamisi, pia siku maalum ya wanawake duniani, na kushuhudiwa na wasanii wakubwa nchini ambao wamekuja kumuona.

Amesema mwanaye atajulikana kwa jina la Nabil au Cloud Junior. Pia amepanga mwanaye huyo kumfanyia sherehe kidogo ya kumtoa ya siku ya saba, kisiwani Zanzibar ambapo yeye alizaliwa.

Cloud 112 na mkewe walitembelewa na wadau wengi wa Bongo Movie ambao walifika kutoa baraka na hongera zao. Pia walipata nafasi ya kusema Duwa kwa ajili ya Nabil aka Cloud Junior:
[youtube]http://www.youtube.com/watch?v=JT_NGwUjMhw[/youtube]

Cloud 112 anakuwa anatimiza mtoto wa tatu baada ya wawili kuishi Zanzibar aliyezaa na mke wake wa mwanzo.
Nasi kaama Bongo5 tunamtakia Nabil maisha marefu mema yenye khery na barka tele.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents