Habari

Familia yapata utata kupanda ndege na keki ya birthday

Kampuni ya ndege ya JetBlue inazidi kuwa katika visa na mkasa vya kuwapiga na kuwanyanyasa wateja wao wawapo kwenye ndege.

Hivi karibuni kampuni hiyo ya ndege imejikuta ikiingia katika vichwa vya habari upya baada ya kuwafanyia fujo familia ya watu wanne waliokuwa katiaka ndege hiyo waliokuwa wakielekea New Jersey.

Familia hiyo ya bwana Cameron Burke, na mkewe Minta na watoto wao walikuwa wakifanya suprise party ya birthday , walishindwa kusherekea siku hiyo baada ya maafisa wa ndege hiyo kuwakataza kukata keki kwa kigezo cha usalama wa ndege.

Hata hivyo familia hiyo kupitia baba huyu iliambia kituo cha television cha ABC7 kuwa wao walifuata utaratibu wote kuhusu kupanda na keki na kutaka kusherekea sherehe hiyo.

https://youtu.be/cOdpiRY0Gc4

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents