Uncategorized

Guardiola afunguka ‘Kama tutapoteza dhidi ya Liverpool tumekwisha, ubingwa ndiyo basi tena’

Pep Guardiola anaamini Manchester City nilazima imfunge Liverpool siku ya Alhamisi ili kubaki kwenyembio za kuwania ubingwa wa ligi kuu Uingereza.

Meneja huyo wa City, Guardiola amesema kuwa ushindi pekee siku ya Alhamisi ndiyo utawapa matumaini ya kuendelea kuwania ubingwa.

“Kwanafasi yetu na Liverpool, kama tutapoteza pointi ndiyo basi tena, tumekwisha inamaana itakuwa haiwezekani,’’ amesema Guardiola kwenye mkutano wake na waandishi wa habari.

“Bilashaka hata wao watapoteza pointi lakini hazitokuwa nyingi, kama unahitaji kuwa kileleni ni lazima tukumbuke msimu uliyopita.’’

“Hatupaswi kusahau tupowapi, wakati fulani unalazimika kuwa na sura ya tofauti na kuwa msumbufu kidogo kwa wachezaji na kuwauliza nini kimetokea ?,’’

“Pengine kunasehemu nakosea lakini wachezaji wote wanapaswa kufanya vizuri.’’

City imeshindwa kuwa na muendelezo mzuri wa matokeo licha ya kuibuka na ushindi wa mabao 3 – 1 dhidi ya Southampton siku ya Jumapili wakati magoli hayo yakifungwa na David Silva, Sergio Aguero na James Ward-Prowse.

Ushindi huo unaifanya timu hiyo kwenda kwenyemchezo wake na Liverpool utakao pigwa kwenye dimba la Etihad huku wakishikana fasi ya pili kwa kuzidi wa pointi saba na majogoo hao wa Uingereza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents