Uncategorized

Hisa za Manchester United zapanda ghafla baada ya kutimuliwa Jose Mourinho

Thamani ya klabu ya Manchester United imeongezeka kwa zaidi ya asilimia sita majuzi siku ya Jumanne na kukadiriwa kuwa ni wastani wa pauni milioni 120.

Image result for Mourinho Surprised

Maamuzi ya klabu hiyo ya kumtimua kazi meneja wake Jose Mourinho kumeonyesha kuzaa matunda kwa upande mwingine baada ya kupanda kwa spidi kubwa hisa zake kwa zaidi ya asilimia hizo sita inayokadiriwa kuwa na wastani wa pauni milioni 120.

Safari ya Mreno huyo ndani ya Old Trafford ilihitimishwa kwa kichapo cha mabao 3 – 1 dhidi ya Liverpool kwenye mchezo wa ligi kuu Uingereza.

Mara baada ya tukio hilo thamani za hisa zilipanda mapema mno katika ‘New York Stock Exchange’ kutoka dola 17.30 sawa na pauni 13.65 Jumatatu hadi kufikia dola za Kimarekani 18.39 kwa hisa sawa na pauni 14.51 na bado zinaendelea kuongezeka thamani tangu kuondoka kwa Mourinho hii inakuja hasa kutokana na watu kuamini kuwa pafomansi ya timu hiyo itaimarika.

Manchester United ilipoteza theluthi ya thamani yake ambayo ni sawa na dola za Kimarekani bilioni moja au pauni 800,000 tangu mwanzoni mwa mwezi Agosti.

Ikapanda kwa dola 27.20 ilipofika Agosti  27 ambaposawa na dola za Kimarekani bilioni 3.1 lakini ikashuka tena kwa asilimia 22 na kufikia dola 21.12 sawa na pauni 16.67 Oktoba 1.

United imecheza michezo minne pasipokufungwa, ikiwemo ushindi wa mabao 3-2 dhidiya Newcastle na ushindi wa 2-1 mbele ya Bournemouth.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents