Uncategorized

Hivi ndivyo ilivyokuwa kwenye ‘Derby’ ya Panathinaikos dhidi ya Olympiacos (+video)

Vurugu kubwa zimeripotiwa kujitokeza kwenye mchezo wa Derby ya Panathinaikos dhidi ya Olympiakos hapo jana siku ya Jumapili ligi ya Ugiriki maarufu kama Greek Super League baada ya mashabiki wa Panathinaikos kufanya vurugu iliyopelekea hadi askari Polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya.

Mashabiki wa Panathinaikos wakiwa nyumbani kwenye dimba lao la
 OAKA Stadium walianzisha vurugu hizo kwa kushambulia wachezaji wa
Olympiakos waliyokuwa ndani ya uwanjani pamoja na mashabiki.

https://www.youtube.com/watch?v=d0coA6jtbMw

Kufuatia vurugu hizo zilizotawaliwa na mabomu ya machozi nje ya uwanja ilipelekea mwamuzi wa Kijerumani, Marco Fritz kusimamisha pira kwa zaidi ya dakika tano ilipofika dakika ya 70.

Hata hivyo wageni, Olympiakos walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1 – 0 dhidi ya wenyeji wao Panathinaikos baada ya mchezaji
Miguel Angel Guerrero kuifungia timu yake dakika ya 53.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents