Uncategorized

Huyu ndiye mtoto mwenye kasi zaidi, akiwa na miaka 7 pekee anatarajiwa kuvunja rekodi ya Usein Bolt (+video)

Rudolph Ingram Jr maarufu kama ‘Blaze’ ni mtoto mwenye umri wa miaka saba na alianza kukimbia akiwa na miaka mitatu pekee baada ya kuangalia mashindano ya Olimpiki na babake.

Blaze kwa sasa huwenda akawa mtoto mwenye kasi zaidi katika mchezo wa riadha, hii ni kutokana na kukimbia mbio za mita 100 kwa sekunde 13,48 tu na kuingia kwenye vitabu vya rekodi nchini Marekani kwa watu wenye umri wake.

https://www.instagram.com/p/Bs-yFgxB-AC/

Wachambuzi wa mambo wanaamini Blaze ndiye mtu atakayekuja kuvunja rekodi iliyowekwa na mwanariadha mwenyekasi zaidi duniani Usein Bolt ambaye amewahi kukimbia mita 100 kwa 9.69 kwa sekunde.

“Najivunia usema kuwa mtoto wangu huwenda akawa ndiye mkimbiaji zaidi kwa watu wenye umri kama wake duniani, muda wote anapenda kufanya mazoezi ya kukimbia na kuonyesha kwenye akaunti yake ya Instagram,” amesema baba mzazi wa mtoto huyo.

Baba wa kijana huyo ameongeza ”Wakati akiwa na umri wa miaka mitatu, tulikwenda kuangalia mashindano ya Olimpic, na palivyokucha siku ya pili alianza kufanyia kazi kile alichokiona, na kuanzia siku hiyo amekuwa mtoto mwenye kasi kubwa zaidi kwenye eneo hili.”

”Anafahamu kuwa yeye ndiye mshindani wake binafsi, kwa hiyo anakimbia dhidi yake.”

https://www.instagram.com/p/BtcfzG5hU0-/

Kwa mujibu wa baba mzazi wa mtoto huyo, Rudolph Ingram Sr ambaye ni kocha wa mchezo wa soka nchini Marekani amesema kuwa Blaze alianza kuvutiwa na riadha akiwa na miaka mitatu tu baada ya kutembelea mashindano ya Olimpic.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents