MichezoUncategorized

Kesi za viongozi wa TFF na Simba zaendelea kupigwa kalenda

Kesi zinazowakabili viongozi wa TFF na ile inayowakabili viongozi wa klabu ya soka ya Simba zimeendelea kuahirishwa tena leo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Katika kesi ya kwanza inayomkabili Rais wa TFF, Jamal malinzi, Mwesigwa Selestine na Nsiande Isawafo kutokana na makosa ya matumizi mabaya ya madaraka waliyokuwa nayo katika uongozi wao imesogezwa mbele kutokana na uchunguzi wa kesi hiyo kutokamilika.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi August 11 ya mwaka huu.

Katika kesi nyingine inayomkabili rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva na makamu wake, Godfrey Nyange maarufu Kaburu imeahirishwa katika mahakama hiyo baada ya uchunguzi kutokamilika na imepangwa kusikilizwa tena Jumatatu ya wiki ijayo ya August 7.

Aveva na Kaburu wanakabiliwa na tuhuma za kughushi nyaraka za Simba SC na kutakatisha dola 300,000 (zaidi ya Sh milioni 650) na wamekuwa mahabusu tangu Juni 29, mwaka huu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents